Kwa nini Kelechi akageukia utayarishaji wa mziki

July 1, 2018

Msani Kelechi Africana amefichua sababu kwa nini alijifunza jinsi ya kutayarisha mziki badala ya kuendelea kuwa mwanamuziki pekee.

Kulingana na msanii huyo kutoka pwani ni kuwa watayarishaji wengi wa mziki walikuwa wakibania kazi yake jambo ambalo lilimfanyakujifunza utayarishaji.

“Nilifanya zaidi ya ngoma kumi lakini kila produsa alikuwa anabania kazi yangu, mara naambiwa ngoma ilifutika mara ni kirusi kimekula kazi yangu, hali hii ilinisukuma zaidi nijifunze kuwa produsa,” amesema Kelechi.

Kwa sasa msanii huyo anatingisha anga kwa ngona “Wapoteze”

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.