Afikishwa mahakamani kwa kushika makalio bila idhini

December 5, 2017

Mahakama ya mjini Kwale imemuachilia kwa dhamana ya shilingi laki mbili au pesa taslimu shilingi elfu 50 mwanamume mmoja kwa kumkosea heshima mwanamke.

Inadaiwa kuwa mnamo tarehe 3 mwezi Disemba mwaka huu, mwanamume huyo kwa jina Suleiman Hamisi alimshika makalio na matiti mwanamke huyo bila idhini akiwa katika eneo la mteza mbuguni kaunti ya Kwale.

Mahakama imetaja kitendo hicho kama cha kumkosea adabu mwanamke huyo.

Akiwa mbele ya hakimu Doreen Mulekyo, mwanamume huyo amekanusha shtaka hilo huku kesi hiyo ikipangwa kusikizwa tena tarehe 30 mwezi Januari mwaka ujao.

Taarifa na Mimu Mohammed.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.