AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UWINDAJI HARAMU

December 4, 2017

Mwanamume mmoja amefikishwa katika mahakam aya Kwale kujibu shtaka la uwindaji haramu.

Inadaiwa kuwa tarehe 2 mwezi Disemba mwaka huu, mwanamume huyo kwa jina Mriphe Vuo Mtundo alipatikana na vipande vya nyama ya Swara vyenye uzani wa kilo 13 huko Burani Mwaluphamba kaunti ya Kwale.

Wakitoa ushahidi wao, maafisa wa shirika la huduma kwa wanyamapori KWS wameiambia mahakama kuwa jamaa huyo aliua swara wawili.

Akiwa mbele ya Hakimu Doreen Mulekyo mshtakiwa amekubali kosa hilo na akahukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani ama faini ya shilingi laki 4.

Taarifa na Mimu Mohammed

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.