Agina alenga kushinda dhahabu ya Olympiki

November 14, 2017

Baada ya kuonyesha mchezo wa hali ya juu kwenye mkondo wa tano wa ligi ya ndondi nchini bondia Brian Agina analenga kushinda medali katika michuano ya Olympiki.

Bondia huyo kutoka kwa klabu ya Mbaraki, 18,  aliyewakilisha Coast Combined katika mashindano hayo  alimduwaza bondia Morris Ochieng wa kenya Police alipomtandika 3-0 kwenye mechi ya uzani wa Fly wikendi.

Akizungumza na meza yetu ya michezo Agina amesema kuwa anamatumaini makubwa ya kufika Olympiki baada ya kuwa bingwa chipukizi nchini kwa miaka mitatu mfululizo.

“Lengo langu kuu ni kuchezea Kenya katika michuano ya Olympiki ili niweze kuishindia Kenya dhahabu halafu nigeukie ndondi ya kulipwa,” amesema Agina.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.