Chama cha ODM kupitia kamati ya nidhamu ya chama hicho sasa kinataka Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa na mwenzake wa Msabweni Suleiman Dori wafurushwe kwenye chama hicho.
Katibu wa chama hicho Edwin Sifuna amesema kuwa wawili hao pamoja na wawakilishi 6 wa wadi kutoka kaunti za Homa Bay na Busia wanafaa kufurushwa chamani kwa kutofuata masharti ya chama hicho sawa na kutomuheshimu kinara wao Raila Odinga.
Pendekezo hilo linajiri baada ya Aisha, Dori na wawakilishi hao kutangaza hadharani azma yao ya kumuunga mkono Naibu wa rais William Ruto kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2022.
Hatima ya wawili hao sasa inasalia mikononi mwa kamati kuu ya ODM ambayo itaidhinisha iwapo wafurushwe chamani au la.
Taarifa na Mimu Mohammed.
Viongozi wa kaunti ya Mombasa wakosoa kupunguzwa kwa mgao wa fedha
Baadhi ya viongozi wa kaunti ya Mombasa wameikosoa hatua ya serikali kuu kwa kupunguza mgao wa fedha wa bajeti ya mwaka wa 2019/2020 kwa kaunti hiyo kwa asilimia 12.
Uongozi duni watajwa kuwa chanzo cha kukosekana kwa maendeleo
Mwanaharakati wa masuala ya kisiasa mjini Mombasa Ali Mwatsahu amesema maeneo bunge ya kaunti ya Mombasa yamekosa kujiendeleza kimaendeleo kutokana na uongozi duni.