Aliyekwenda kwa Ali Kiba sasa asema yuko Kiganjani

December 1, 2017

Mambo ya msanii Grace Mueni maarufu kama Ngunash, aliyejibu shairi la Ali Kiba “Aje” yanazidi kunoga.

Wawili hao walikutana kipindi cha uchaguzi humu nchini na kulingana na Ngunash walikuwa na muda mzuri pamoja.

Baada ya wakati huo mzuri, Ngunash ameachilia kitu ambacho kimezua atiati miongoni mwa mashabiki wake.

Msanii huyo ameachilia shairi jipya kwa jina Kiganjani. Katika shairi hilo anaelezea jinsi alivyolewa na penzi la bwana mmoja. Ni nani huyu aliyemlewesha na mahaba ? Je ni Ali Kiba?

Jibu unalo katika video hii.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.