Exclusive: Amarila alia mwani licha ya kufanya vyema kimziki

November 29, 2017

Picha/ kwa hisani ya Amarila

Unaposikia nyimbo Chocha, Nichomeshe au Demu la Kienyeji bila shaka jina Amarila linakujia kichwani.

Kando na kulifahamu jina hili ubora wa video za nyimbo hizi zitakupa sifa ya msanii aliyefanikiwa kimziki kufikia sasa. Ukweli wa mambo hata hivyo ni kuwa licha ya kutawala anga na mziki wake Ali Rama maarufu kama Amarila hajapata faida yoyote kutokana na mziki wake.

“Amarila maisha yake ya mziki yako tofauti na yake yanayojulikana katika media kwa sababu niko katika hali ya kusaidiana pale mahali nipo … kwa hivyo siezi kusema kuwa Amarila amefaidika katika mziki kufikia saa hizi… hela bado sijaangukia,”amesema Amarila.

Msanii huyo aidha amesema kuwa yupo tayari kufanya biashara na mtu yoyote atakayeamua kumshika mkono ili kupata faida kutoka kwa mziki wake. Sikiliza mahojiano kamili hapa.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.