Arnold Origi akuza vipaji Kwale

January 5, 2019

Arnold Origi akipeana vifaa vya michezo kwa watoto Kwale.

Arnold Origi akipeana vifaa vya michezo kwa watoto Kwale.

Aliyekuwa kipa wa timu ya taifa soka nchini Harambee stars Arnold Origi, ameihimiza jamii ya kaunti ya Kwale  kukuza talanta ya michezo miongoni mwa watoto  ili kuwaepusha na   visa vya uhalifu na utumizi wa mihadarati.

Akiongea  katika uwanja wa michezo ya Kombani alipokutana na  watoto  wenye umri  chini ya miaka 12 wanaochezea timu mbalimbali  kupitia udhamini wa shirika la Samba Sports, Origi  amewapa wazazi changamoto  kutambua vipaji  vya watoto wao na kuvikuza.

Amesema kuwa  maeneo ya miji  ikiwemo Nairobi ikiendelea  kuwapa watoto motisha wa  kuboresha vipaji vyao katika michezo,  maeno ya mashimani yangali yamesalia nyuma, huku akiongeza kuwa   ameanza kuzuru sehemu hizo za mashinani,  kuhamasiha jamii kuhusu umuhimu wa michezo.

Mchezaji huyo  aidha amedokeza kuwa  mbali na   kufungua mlango wa  maendeleo maishani,  michezo inaweza kutumika kama kampeni ya kuwahamasisha vijana kuhusu athari za  makundi ya kihalifu, utumizi wa mihadarati , mimba na ndoa za mapema miongoni mwa wasichana wadogo.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.