Asilimia 80 ya watu hawajui jinsi ya kupiga kura Kinango

August 4, 2017

Zikiwa  zimesalia  siku  3  tu  kabla  ya  uchaguzi  mkuu,  imebainika  kuwa  zaidi ya  asilimia 80  ya  watu  katika  eneo bunge la Kinango kaunti ya Kwale hawajafahamu  jinsi  ya  kupiga  kura.

Kulingana na Msimamizi  wa  Uhamasisho  wa  upigaji  kura  eneo  la  Kinango  Abraham Wekesa  Masinde ni  kwamba  hali  hiyo  ilichangia  kuharibika kwa   kura nyingi   katika  uchaguzi  mkuu  uliopita.

Afisa  huyo  aidha  amesema  kuwa  wazee  kukatalia  vitambulisho  vya  wake  zao au  kuwalazimisha  kuwapigia  kura  wagombea   au  vyama  fulani ni  baadhi  ya  mambo  yanayodidimiza  hamasa  kuhusu upigaji  kura  katika  eneo  hilo.

Wekesa  amewataka  viongozi  wa  kisiasa  kukoma kutoa hamasa  kuhusu  upigaji  kura  akisema  huenda  watawapotosha  wapiga  kura.

Taarifa hii imeandikwa na Lucy Makau.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.