Babkubwa, mwanamziki anayelinda hadithi za Wamijikenda

December 4, 2017

Ni lengo la wanamuziki wengi kuwa na umarufu na kupata hela kutokana na kazi yao ya kisanii.

Licha ya hilo kuwa miongoni mwa malengo ya msanii Kahindi Fundi, binafsi yupo na lengo kuu linalomfanya tofauti na wanamuziki wengine Wapwani.

Kwa ushirikiano na kundi la Chondoni ameanza harakati za kuhifadhi hadithi na historia ya wamijikenda kupitia nyimbo.

“Nilitaka wajukuu zangu wasiikose historia ya wamijikenda kwa sababu kwa sasa kila kitu kina badilika haraka. Ukiangalia mavazi yetu tayari yamepitwa na wakati ndio maana nikaamua kuzihifadhi historian a hadithi za wamijikenda  katika nyimbo,” amesema Babkubwa.

Kwa sasa msanii huyo anayetokea Malindi ametoa kanda moja kwa jina Chondoni iliyo na nyimbo kumi, miongoni mwa nyimbo hizo ni Chondoni ambapo ameimba kuhusu hadithi ya Mbodze na Matsedzi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.