BAK yailaumu serikali kwa kujiondoa kwa SportPesa

January 2, 2018

Shirikisho la mchezo wa ndondi nchini Kenya Boxing Association (BAK) limeilaumu serikali kwa kuchangia kujiondo kwa kampuni ya Sport Pesa iliyokuwa ikifadhili mchezo huo humu nchini.

Rais wa shirikisho la mchezo huo nchini John Kamete amesema kwamba hatua ya bunge la kitaifa kupitisha sheria mwishoni mwa mwaka jana ya kuzitaka kampuni za michezo ya bahati nasibu kulipa asilimia thelathini na tano ya mapato yake ndiyo iliyochangia kujiondoa kwa wadhamini hao.

Akizungumza na wanahabari kamete amedokeza kwamba hatua hiyo itaathiri pakubwa ukuaji wa mchezo huo kwani shirikisho hilo lilitegemea pakubwa wadhamini hao kuendesha ligi ya mchezo huo.

Kamete aidha ameilaumu serikali pamoja na wizara ya michezo nchini kwa kukosa kuwajibikia vyema masula ya michezo humu nchini.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.