Balozi wa marekani awataka wanasiasa kutoingilia utendakazi wa mashirika ya kijamii

August 25, 2017

Balozi wa Marekani nchini Robert Godec amesema kuwa mashirika ya kijamii yanapaswa kupewa fursa ya kutekeleza majukumu yao  bila kuingiliwa kisiasa.

Katika mahojiano ya kipekee na Radio Kaya, Godec amedokeza kuwa  mashirika hayo  yamechangia pakubwa maendeleo katika jamii, huku akisisitiza kuwa juhudi zao zinahitaji kuungwa mkono na serikali na jamii kwa jumla.

Balozi huyo ameeleza  kuwa  mashirika ya kijamii  nchini  yameboresha huduma  za afya, elimu na vile vile utetezi wa haki za binadamu hatua anayosema imeimarisha maisha ya wananchi mashinani.

Kauli ya Godec inajiri siku chache tu baada ya  bodi inayosimamia mashirika yasiyo ya kiserikali kuipokonya leseni tume ya kutetea haki za binadamu nchini (KHRC) na afisi za shirika la AFRICOG kuvamiwa na maafisa wa halmashauri ya utozaji ushuru nchini KRA. Hata hivyo kaiumu waziri wa usalama wa ndani Dakta Fred Matiang’i alibatilisha hatua hiyo na kuagiza pande zote husika kujadiliana na kisha kutoa ripoti yao kwa muda wa siku 60.

Taarifa hii imeandikwa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.