Bandari kupambana na Kariobangi Sharks fainali

January 25, 2019

50688965_590731928032551_1139063779741401088_o

Klabu za Bandari FC na Kariobangi Sharks zitakutana kwenye fainali ya michuano ya SportPesa Super Cup siku ya Jumapili.

Bandari imeibandua Simba kutoka Tanzania kwenye michuano hiyo kwa ushindi wa goli 2-1 na kujipatia tiketi ya kuingia fainali.

Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Meddie Kagere kunako kipindi cha kwanza. Magoli yote ya Bandari FC yamefungwa kipindi cha pili kupitia kwa Wyclif Ochomo na William Wadri aliyefunga penanti yake ya pili katika pambano hilo.

Matumaini ya Watanzania yamedidimia pale Kariobangi Sharks walipowabandua Mbao FC kupitia mikwaju ya penanti 6 – 5 baada ya kutoka sare katika muda wa kawaida.

Mshindi kati ya Bandari FC na Kariobangi Sharks atacheza dhidi ya Everton ya Uingereza.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.