Bandari waandikisha Sare dhidi ya Mathare

May 12, 2018

Picha/ kwa hisani

Klabu ya Bandari imetoka sare ya kutokufungana na klabu ya Mathare United.

Mechi hiyo imesakatwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Kabla ya Ngarambe hiyo mkufunzi wa Badari Ken Odhiambo aliambia vyombo vya habari kuwa walikuwa wanalenga kupata ushindi katika mechi hiyo.

Na matokeo haya klabu ya Bandari inaujumla wa pointi 24.

Kwa sasa Bandari wanajiandaa kwa ajili ya mechi ya nyumbani dhidi ya Posta. Mechi hiyo itachezwa tarehe 19 Mei.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.