Bandari walenga kuwanyamazisha Mathare

May 12, 2018

BANDARI 05 02 18

Baada ya kulimwa nyumbani na klabu ya Tusker sasa klabu ya Bandari inalenga kulipiza kisasi dhidi ya Mathare United.

Timu hizo mbili zinakutana mchana wa leo kuanzia saa nane mchana katika uga wa Kenyatta mjini Machakos.

Kulingana na mkufunzi mkuu wa Bandari Ken Odhiambo mechi hii ni lazima washinde ili kujinasua kutoka kwa aibu ya kushindwa nyumbani.

Bandari walichapwa mabao 2-0 nyumbani wikendi iliyopita.

Jumamosi Mei 12

Mathare United vs Bandari – 2PM – Machakos

AFC Leopards vs Nakumatt – 4:15PM – Machakos

Sofapaka vs Zoo FC – 3PM – Narok

Jumapili Mei 13

Thika United vs Sony Sugar FC – 3PM – Thika

Kakamega Homeboyz vs Chemelil Sugar FC – 3PM – Bukhungu

Vihiga United vs Wazito FC – 3PM – Mumias

Tusker FC vs Kariobangi Sharks – 3PM – Ruaraka

Posta Rangers vs Nzoia Sugar FC – 3PM – Camp Toyoyo

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.