Bandari watoa onyo kali kwa Gor Mahia

October 29, 2018

BANDARI

Afisaa Mkuu Mtendaji wa klabu ya Bandari, Edward Oduor ametoa onyo kali kwa wanaommezea mate mchezaji Hassan Abdalla.


Onyo hilo limeelekezwa kwa klabu ya Gor Mahia baada ya taarifa kuibuka kuwa k’Ogallo wanamnyapia nyapia mchjezaji huyo.
Edu ametoa onyo hilo baada ya habari kusema kuwa Lordick Aduda wa Gor Mahia alikuwa mjini kutafuta saini ya Hassan.
Abdalla ni mchezaji kinda katika klabu ya Bandari ambaye ameonyesha makali yake hususan katika kasi ya mchezo.
Klabu ya Bandari ndioyo timu ya kwanza kumaliza ubabe wa Gor Mahia wa kutoshindwa kwa kuichapa mabao 2-1 nyumbani msimu uliopita.
Tarehe 8 Disemba Gor Mahia na Bandari wanakutana katika uga wa KPA Sports Club Mbaraki.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.