Bandari yaingia fainali ya SportPesa Super Cup

January 25, 2019

Klabu ya Bandari imeibandua Simba kutoka Tanzania kwenye michuano ya SportPesa Super Cup kwa kipigo cha goli 2-1.


Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Meddie Kagere kunako kipindi cha kwanza na magoli yote ya Bandari FC yamefungwa kipindi cha pili.

Matumaini ya Watanzania kwa sasa yamebakia kwa Mbao FC pekee, kwani tayari Klabu ya Simba, Singida United na Yanga zimeshatupwa nje ya michuano hiyo ambayo mshindi atacheza na Everton ya Uingereza.

Bandari FC kwa sasa imetinga fainali na itasubiri mshindi wa mechi ya baadae kati ya Kariobangi Sharks na Mbao FC.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.