Bandari yampiga kalamu Nkata

December 1, 2017

Mkufunzi wa klabu ya Bandari ametangaza kuwa anaondoka klabuni humu baada ya kuhudumu kwa miezi 12.

Mganda huyo alijiunga na klabu ya Bandari mwezi Disemba mwaka 2016 baada ya kutajwa mkufunzi wa mwaka pale alipowasiadia Tusker kushinda mataji mawili msimu huo.

Chini ya uongozi wake klabu ya Bandari imemaliza msimu katika nafasi ya 10 ikiwa na alama 43.

Mkufunzi huyo amesema kuwa ameachana na klabu hiyo katika uhusiano mzuri na yuko tayari kumwaga wino na klabu nyingine iwapo itakuwa na ofa nzuri kwake.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.