Bandari Youth waibuka mabingwa Mombasa

November 27, 2017

klabu ya Bandari Youth ndiyo mabingwa wa mwaka huu wa ligi ya Premia ya Mombasa.

Bandari wamenyakua taji hilo kwa kuandikisha ushindi mnene wa mabao 4-2 dhidi ya Wanderers FC kwenye mechi iliyochezwa katika uwanja wa KPA Mbaraki Sports Club.

Kwa ujumla Bandari Youth walikusanya pointi 89. Wananyuki FC walimaliza katika nafasi ya pili na alama 76, nafasi ya tatu iliwaendea Omax FC waliojinyakulia pointi 65.

Klabu za Miritini Warriors, Bamburi United na Eleven Stars zinadondoka kutoka kwa ligi hiyo huku nafasi zao zikichukuliwa na klabu za Boca Junior walioshinda ligi ya daraja la kwanza wakiwa na alama 44, Miritini Youngstars waliokuwa wapili kwa alama 41 na Redemption waliokuwa watatu kwa  alama 41.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.