Bi Mboko awalaumu polisi walafi Likoni

December 11, 2018

Mbunge wa Likoni bi. Mishi Mboko amedai kwamba baadhi ya maafisa wa polisi katika eneo hilo huchukua hongo kutoka kwa walanguzi wa dawa za kulevya hali inayochangia ongezeko la visa vya uhalifu katika eneo la Likoni.

Mboko amehoji kuwa maafisa hao wanaregesha nyuma juhudi zinazoendelezwa kufanikisha vita dhidi ya ulanguzi na utumizi wa mihadarati sawa na uhalifu katika eneo hilo.

Amesema kuwa iwapo  idara ya usalama inalenga kufanikisha vita dhidi ya uhalifu unaochangiwa na vijana wanaotumia mihadarati ni sharti maafisa wanaochukua hongo kutoka kwa walanguzi  wakabiliwe.

Mbunge huyo aidha ameongezea kuwa usalama utaimarika  zaidi katika eneo hilo endapo idara ya usalama itawakabili walanguzi wadogo wadogo wa dawa za kulevya.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.