Bilioni 80 kutumiwa katika ujenzi wa daraja Likoni

December 8, 2017

Serikali kuu kwa ushirikiano na Serikali ya Japani wanapania kujenga daraga la kisasa katika eneo la kivuko cha Feri cha Likoni ili kupunguza msongamano wa mara kwa mara katika kivuko hicho.

Kulingana na Afisa anayesimamia ujenzi wa daraja hilo Michael Mwangi, ujenzi huo utaanzia katika eneo la Jela baridi huko King’orani kaunti ya Mombasa hadi maeneo ya ziwani kaunti ya Kwale.

Mwangi amesema kuwa daraja hilo la kisasa litagharimu kima cha shilingi bilioni 80 huku akifichua kuwa ujenzi huo huenda ukachukua mda wa miaka ya 4 kwani litakuwa daraga la urefu wa kilomita 1.4.

Wakati uo huo amehoji kuwa ujenzi wa daraja hilo hautaathiri shughuli za kivuko hicho cha Likoni na Mtongwe huku akidai kuwa utaimarisha zaidi uchumi na biashara kanda wa Pwani.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.