Bodi ya filamu kuandaa tamasha kubwa Malindi

December 8, 2017

Wadau wa Sekta ya Utalii humu nchini wakishirikiana na Bodi ya filamu nchini, sasa wanapanga kuandaa tamasha la kimataifa la filamu mjini Malindi kama njia moja wapo ya kufufua sekta ya utalii hapa Pwani.

Tamasha hiyo ya filamu inatarajiwa kufanyika Disemba mwaka wa 2018, tamasha ambalo limeratibiwa na Waziri wa Madini nchini Dan Kazungu kwa lengo la kuifufua sekta ya Utalii.

Akizungumza na Wanahabari mjini Malindi baada ya kutembelea hoteli mbalimbali zikazoandaliwa tamasha hilo huko Malindi, Mkurugenzi mkuu wa Bodi hiyo Ezekiel Mutua amesema kuwa tamasha hilo litafungua milango ya kimataifa ya wageni kuzuru eneo la Pwani.

Kwa upande wake Waziri wa madini Dan Kazungu amesema kuwa watashirikiana na wadau mbali mbali wa sekta ya utalii sawia na bodi ya utalii nchini ili kuhakikisha sekta ya utalii inaimarishwa.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.