Bodi ya filamu yaombwa kuwachukulia hatua wanaopotosha watoto mitandaoni

June 28, 2018

Afisa anayesimamia masuala ya watoto katika Kaunti ya Mombasa Philip Nzenge ameitaka bodi ya filamu nchini kuliangazia suala la watoto wadogo kunajisiwa kupitia mitandao ya kijamii na kuwachukulia hatua wahusika.

Akiongea mjini Mombasa Nzenge amesema kuwa visa hivyo vimekithiri katika kaunti hiyo na maeneo mengine nchini ukizingatia kwamba watoto wengi hutumia mitandao ya kijamii pasi na ufahamu wa wazazi wao.

Afisa huyo vile vile amewalaumu wazazi kwa kutofatilia mienendo ya watoto wao hali ambayo amesema kuwa imechangia pakubwa kuongezeka kwa visa hivyo.

Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa shirika la Children Kenya Martha Sunda amesema tayari shirika hilo linaendeleza hamasa kwa watoto kuhusu athari za mitandao ya kijamii ilikuwaepusha kutendewa  unyama huo.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.