Bondia wakenya atoweka kambini, Australia

April 16, 2018

OMOLLO MAU KSM VS ANTHONY KARIUKI KONGOWEA

Bondia kutoka Pwani aliyeshiriki katika mashindano ya Jumui  ya Madola, Brian Agina ameripotiwa kupotea nchini Australia.


Bondia huyo anaripotiwa kuondoka kutoka kwa kijiji cha michezo hiyo jumapili usiku.

Kulingana na rais wa muungano wa mchezo wa Ndondi nchini John Kameta tukio hilo limeripotiwa kwa mkuu wa kikosi cha kenya Barnabas Korir na vilevile kwa maofisaa wa polisi ambao tayri wameanzisha msako.

Polisi nchini humo wanawatafuta wanamichezo wawili waliopotea.

Wiki iliyopita jumla ya wanariadha wanane kutoka nchini Cameroon pia walitoweka kambini.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.