BUNGE LA KAUNTI YA KWALE KUSHUGHULIKIA TATIZO LA MAJI

December 5, 2017

Kamati ya bunge la kaunti ya Kwale kuhusu masuala ya Maji na Afya imeahidi kulishuhulikia swala la uhaba wa maji katika kaunti ya Kwale.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mwakilishi wa Wadi ya Waa, Mwinyi Mwasera amesema kuwa tayari mikakati inaendelea ya kulitatua tatizo hilo.

Mwasema amesema kuwa japo kaunti ya Kwale ina raslimali na maji ya kutosha lakini cha kushangaza bado wakaazi wa kaunti hiyo wanapitia changamoto huku akisema kuwa swala hilo litajadiliwa katika bunge la kaunti hiyo.

Mwasera ametaja kuwa mbali na masuala ya maji kugatuliwa kumekuwa na vuta ni kuvute baina ya bodi ya maji ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale na akaahidi kupigania ugavi sawa wa bidhaa hiyo.

Taarifa na Mariam Gao

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.