Bunge la kaunti ya Kwale lapitisha mswada wa bunge la mwananchi

November 29, 2017

Hatimaye bunge la kaunti ya Kwale limekuwa bunge la kumi nchini kupitisha mswada wa kuunga mkono uwepo wa bunge la wananchi.

Mswada huo umewasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wengi katika bunge la kaunti ya Kwale Joseph Ndeme ambaye amesema kuwa kulikuwa na umuhimu wa kupitishwa kwa mswada huo ikizingatiwa kuwa wananchi wa Kwale wamekuwa wakinyanyashwa.

Wajumbe wa mrengo wa Jubilee, Wakiongozwa na Antony Yama wamesusia kikao cha kupitisha mswada huo katika bunge hilo la kaunti ya Kwale wakitaja kuwa hatua hiyo ni kinyume cha sheria

Kwa upande wao wakaazi wa Kwale wanaounga mkono mrengo wa Jubilee, wakiongozwa na Suleiman Mwarundu wamepinga vikali kupitishwa kwa mswada huo.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.