BUNGE LA TAITA TAVETA LAPIGA MSASA MAWAZIRI

December 4, 2017

Bunge la kaunti ya Taita Taveta limewapiga msasa mawaziri wawili walioteuliwa na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja kuchukua nafasi ya wizara ya maji na mwengine wizara ya barabara na muundo msingi.

Wakwanza kufika mbele ya bunge hilo ni Gasper Kabaka ambaye aliteuliwa kama waziri wa maji katika kaunti hiyo, ambapo ameliambia bunge hilo kuwa tatizo la uhaba wa maji limechangiwa na uzembe wa baadhi ya maafisa.

Bunge hilo pia limempiga msasa Houghton Msagha alieteuliwa kama waziri wa nyumba, barabara na miundo msingi katika serikali ya kaunti hiyo, ambapo ameahidi kukarabati barabara za kaunti hiyo zilizo katika hali duni.

Taarifa na Fatma Rashid

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.