Chama cha Jubilee kuvunjwa

January 8, 2019

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha TipTip Kalembe Ndile.

Aliyekuwa kiongozi wa chama cha TipTip Kalembe Ndile.

Huku mgogoro ukiendelea kushuhudiwa ndani ya chama cha Jubilee, baadhi ya viongozi wa vyama tanzu katika chama hicho sasa wanashinikiza kivunjwe.

Akiongea mjini Kwale aliyekuwa kiongozi wa chama cha TipTip Kalembe Ndile, amemtaka rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto, kuvunja chama hicho akisema kuwa kimepoteza mwelekeo.

Kalembe amesema kuwa  licha ya Rais Kenyatta  kuwaonya baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho dhidi ya kuendeleza kampeni za mapema  kuhusu uchaguzi wa mwaka  wa  2022, viongozi hao wamekaidi  onyo la Rais.

Kalembe amepuuzilia mbali mkataba wa  urithi wa  kiti cha urais kati ya Kenyatta na Ruto, akisema kuwa  viongozi wa vyama tanzu vya Jubilee  hawakukubaliana juu ya suala hilo.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.