Chuo kikuu cha Taita Taveta kutoa mafunzo kuhusu madini

November 23, 2017

Zaidi ya mahafala 600 katika vitengo tofauti wamefuzu katika chuo kikuu cha Taita Taveta hii leo.

Akiongea katika zoezi la kufuzu kwa mahafala hao Naibu Chansela katika chuo hicho prof.Hamadi Boga amewapongeza mahafala hao.

Boga ametoa mwito kwa washikadau wote katika sekta ya elimu kushirikiana ili kukiwezesha chuo hicho kuafikia malengo ya kutoa mafunzo bora pamoja na kutoa wanafunzi bora.

Chuo hicho kinalenga kutoa mafunzo bora kuhusu madini  ikizingatiwa kuwa kaunti ya Taita Taveta ina wingi wa madini.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.