CICC yaitaka idara ya usalama kuwapa wananchi ulinzi wa kutosha

August 3, 2017

Baraza la viongozi wa dini tofauti hapa pwani (CICC) limeitaka idara ya usalama nchini kuhakikisha inatoa ulinzi wa kutosha kwa wananchi wakati na hata baada ya uchaguzi mkuu.

Naibu Mwenyekiti wa baraza hilo kanda ya Pwani Shariff Muhdhar Khitamy amesema kuwa wananchi wamekuwa na hofu ya kukumbwa na ghasia hivyo basi idara hiyo inafaa kuweka mikakati mwafaka.

Khitamy ameihimiza idara ya usalama kutoegemea upande wowote wa kisiasa na badala yake iwajibike katika kuwalinda wananchi.

 Khitamy amewahimiza viongozi wa kisiasa kukoma kueneza matamshi ya chuki na uchochezi na kuwataka vijana kujitenga na viongozi wanaonuia kuwatumia kuzua kuvurugu.

Taarifa hii imeandikwa na Cyrus Ngonyo / Picha: Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.