CIPK yaitaka mahakama kufichua waliohusika na sakata ya NYS

July 10, 2018

Baraza la Maimam na Wahubiri wa dini ya kislamu humu nchini CIPK limeitaka Idara ya Mahakama nchini kufichua ukweli kuhusu watu waliohusika na Sakata ya mabilioni ya pesa ya NYS.

Akizungumza na Wanahabari, Katibu mtendaji wa Baraza hilo Sheikh Mohammed Khalifa amesema kuna haja ya kuwepo kwa uwazi kuhusiana na sakata hiyo.

Sheikh Khalifa anasema watu wanaodaiwa kupora mali za umma wamechangia pakubwa kulemaleza shughuli za maendelo nchini huku akiwataka viongozi kushirikiana katika kulikabiliana na ufisadi nchini.

Wakati uo huo amependekeza kuchukuliwa hatua kali za kisheria kwa wale wote waliohusika kwenye sakata ya NYS.

Kwa upande wake Mweka hazina wa Baraza hilo, Hassan Omar ameitaka serikali kuweka wazi kuhusu Sakata ya Sukari bandia na wala sio viongozi kuonekana kulumbana hadharani.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.