Demba aipongeza FIFA kwa kuipiga jeki soka ya wanawake

December 29, 2017

Mwakilishi wa wanawake wa tawi la Pwani Kusini (SCB) la shirikisho la soka nchini (FKF) Diona Demba amepongeza uamuzi wa FIFA wa kuichagua Kenya kuendeleza mradi wa “New Women Development Project”

Akizungumza na vyombo vya habari Demba amesema kuwa mradi huo utakuza  viwango vya soka ya wanawake humu nchini.

Kulingana na Demba Kenya imekuwa ikipata changamoto kubwa katika ufadhili wa soka ya wanawake na mradi huo utakuwa na mchango mkubwa katika kutatua tatizo hilo.

Wiki iliyopita shiriki la soka ulimwenguni FIFA lilitangaza kuwa Kenya itakuwa nchi ya kwanza kutekeleza mradi huo unaolenga kufikia wachezaji soka wa kike milioni 60 ifikiapo mwaka wa 2026.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.