Dogo Richie afichua mipango aliyokuwa nayo marehemu Sam Wa Ukweli

June 7, 2018

Ulingo wa burudani umegubikwa na wingu wa simanzi kuu baada ya msanii Sam Ukweli kufariki.

Msanii huyo aliyefahamika kwa vibao kama vile “Kwetu wapo” amefariki dunia baada ya kuzidiwa ghafla akiwa studio.

Kulingana na Producer wake Steve msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya tumbo.

Akizungumza na Uhondo msanii Dogo Richie ameelezea kushtushwa sana na kifo chake na kufichua kuwa walikuwa na mipango mingi na msanii huyo.

“Amekuwa akinitumia demo za nyimbo zake na tulikuwa tukiandaa ziara yake humu nchini. Vilevile alikuwa anatafuta msanii nyota wa kufanya kazi naye humu nchini,” amefichua Dogo Richie.

Dogo Richie aidha amesema kuwa walikuwa karibu kufanya video ya wimbo aliomshirikisha.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

Unaweza kuzungumza nasi  kupitia:  Twitter @RadioKaya|| Facebook @RadioKaya ||

Instagram @RadioKaya|| SMS 20931.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.