Dogo Richie ageukia uchomaji nyama

May 22, 2018

Je Dogo Richie ameacha mziki na kuanza kazi ya kuuza nyama choma?

Hapana lakini alikuwa akifanya nini katika mkahawa wa kuchoma nyama?

Kupitia kwa ukurasa wake wa Facebook Dog Richie amepakia picha akiwa katika mkahawa wa kuuza nyama choma. Picha ambayo wengi wamedhania kuwa amegeukia uuzaaji nyama.

“Léo nilipokuwa upperhill Nairobi nilishangaa sana kukutana namashabiki wangu Katika mkahawa wachakula…. Kumbe jina limesambaaa sana nimefurahi sana wanajua nyimbo zangu zote nawanadhani MM nimtanzania #FIRE#”

Dogo Richie anavuma na kibao kipya kwa jina FIRE.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.