Dogo Richie kuachilia nyimbo mpya

May 12, 2018

Tunapoanza kuumega mwezi wa Mei wasanii wa Bongo Fleva hawajateremsaha kasi ya kuachilia kazi mpya sawia na wasanii wa Pwani.

Ali Kiba alivunja kimya chake na kibao ambacho kimezua gumzo huku wakosoaji wakisema kuwa ameishiwa na utunzi.

Kambi ya Dance Hall MSA imeachilia riddim mpya kwa jina White Sands ambayo imepokelewa vyema na wengi.

Msani Dogo Richie pia anajitayarisha kutikisa anga na kibao kipya kwa jina Fire. Kibao hicho kitaachiliwa rasmi tarehe 18 Mwezi huu.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.