DOGO RICHIE KUBADILISHA MWENDO

June 2, 2018

17 08 17 DOGO RICHIE

Msanii Dogo Richie amefichua mbinu mpya atakayoitumia katika kuachilia kazi zake.

Richie anayetawala anga na kibao chake “Fire” kwa sasa amesema kuwa mwaka huu anafanya mambo tofauti na ilivyokuwa awali.

Kulingana naye soko la mziki limebadilika hali iliyomfanya kubadilisha mtindo wake wa kuachilia kazi zake.

Akizungumza na Uhondo msanii huyo amefichua kuwa atakuwa akiachilia wimbo pamoja na video yake.

“Mziki umebadilika. Kuna ushindani mkubwa sana na ndio maana imenibidi nibadilishe baadhi ya mambo katika mziki wangu. Kwa sasa sitoachilia wimbo bila video,” amesema Dogo Richie.

Kulingana na msanii huyo mbinu hiyo ni ya kumwezesha kufikia soko jipya.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.