Dori ahimiza Wapwani kushirikiana

September 10, 2018

Mbunge wa Msambweni Suleiman Dori amezitaka jamii za wamijikenda kushirikiana ilikufanikisha masuala mbali mbali ikiwemo maendeleo miongoni mwao.

Akiongea katika hafla ilileta pamoja jamii mbali mbali za Mijikenda mjini Kilifi Dori amesema kuwa iwapo wamijikenda watazidisha uwiano miongoni mwao, eneo la Pwani litaimarika kimaendeleo hasa katika masuala ya kisiasa.

Wakati uo huo amewasihi vingozi wa ngazi mbalimbali kutoka jamii ya mijikenda kushikana na kutafuta suluhu ya matatizo yanayowakumba wapwani.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.