DPP amteua Qurash kuongoza mashtaka ya kesi za ufisadi

December 4, 2018

Mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajji amemteua Khawar Quresh kuongoza mashtaka dhidi ya kesi za ufisadi zinazowakabili viongozi  wa serikali na wale wa idara ya mahakama.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Hajj amesema kuwa amemtea moja kwa moja Quresha aliena makaazi yake nchini London baada ya kukosa mtu sahihi wakuchukua jukumu hilo licha ya  kutangaza wazi nafasi hio.

Hajji vile vile amesema kuwa uteuzi huo umeambatana kikamilifu na vipengele vya katiba sawa na vipengele vya afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma nchini.

Wakati uo huo amesema kuwa kuteuliwa kwa mwendesha mashtaka wa kibinafsi kutasaidia pakubwa kusikilizwa kwa kesi hizo kwa  uwazi zaidi .

Taarifa na Mimu Mohammed.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.