EACC KUCHUNGUZA MALI ZA WAFANYIKAZI WA KAUNTI

December 5, 2017

Tume ya Maadili kupambana na Ufisadi nchini EACC imetangaza kuzichunguza mali zinazomilikiwa na maafisa wa serikali za kaunti, kabla na baada ya kupata nafasi za kuhudumu katika serikali hizo.

Naibu Mwenyeketi wa Tume hiyo Sophia Lepuchirit amesema kuwa ripoti ya hivi maajuzi ya mkaguzi wa fedha za umma nchini Edward Ouko imeweka wazi kuwa wengi wa maafisa wa kaunti wamehujumu ugatuzi.

Akizungumza mjini Wundanyi kaunti ya Taita Taveta baada ya kufanya kikao na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja, Sophia amesema kuwa utumizi mbaya wa raslimali za umma ni sharti ukabiliwe kisheria.

Taarifa na Fatma Rashid

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.