East African Classic Safari Rally yaingia Kwale

November 29, 2017

Mashindano ya magari ya East African Classic Safari Rally inaingia siku yake ya 7 hivi leo.

Magari hayo yameanza katika hoteli ya Neptune kupitia Mwabungo, Kirewe, Kwale, Ukunda, Gazi, Ramisi na kukamilika katika hoteli ya Neptune.

Katika mzunguko wa jana magari hayo yalikuwa katika mzunguko ulio ingia nchini Tanzania. Hii ilikuwa baada ya siku moja ya mapumziko.

Dereva Richard Jackson akisaidiana na Ryan Champion wakiendesha gari aina ya Porsche waliandikisha muda bora wa dakika 19:12. Baldev Charger akisaidiana na Ravi Soni kutoka Kenya waliandikisha muda wa 19.54 sawa na Geof Bell akisaidiana na Timothy Challen kutoka Afrika Kusini waliokuwa wakiendesha gari aina ya Dtsun 260Z, wawili hawa waliandikisha muda bora kati ya mdereva wote kwa ujumla ikiwa ni  dakika 81:54.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.