Fainali ya Safaricom Chapa Dimba yahairishwa

January 12, 2018

Fainali ya mchuano wa Chapa Dimba hapa Pwani imehairishwa kwa wiki moja. Kulingana na mshirikishi wa eneo la Pwani Michael Karanja mabadiliko hayo yamesababishwa na sababu zisizoweza kuepukika.

Mechi hizo ambazo zilikuwa zicheze jumamosi hii zitachezwa tarehe 20 – 21 Januari katika uwanja wa chuo cha walimu cha Shanzu.

Fainali hiyo itahusisha Shimanza Boys kutoka Mombasa, Shimba Hills na Waa Girls kutoka Kwale na St Johns kutoka Kaloleni(Pwani kusini).

Vilevile kutakuwepo na timu ya BreezeHam Boyz na Solwogidi kutoka Malindi, Iqra kutoka Hola na Kilifi Queens kutoka kilifi (Pwani kaskazini).

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.