FASH P AAHIDI KAZI JUU YA KAZI

January 5, 2018

Japo mwaka umeanza kwa mwendo wa kinyonga kwa wasanii wa ukanda wa Pwani msanii Benjamin Thoya Baya maarufu kama Fash P ameamua kuwa tofauti na wasanii wengine mwaka huu.

Akizungumza na Uhondo mkali huyo wa mziki wa kufoka ameapa kuwa mwaka huu atachilia kazi juu ya kazi.

Mwaka uliopita alitikisa anga na ngoma alizomshirikisha Bocar J na Dogo Richie amabazo zilifanya vyema.

Hii ilikuwa afueni kwake baada ya wasanii wakubwa ukanda wa Pwani kumnyima nafasi ya kufanya kolabo naye. Licha ya changamoto hiyo aliweza kupenya na kukubalika na wengi.

Je atazidi kuwa juu mwaka huu?

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.