Feri ya Mtongwe yaanza huduma zake tena

January 10, 2018

Huduma za uchukuzi katika kivuko cha feri cha Mtongwe kaunti ya Mombasa zimerudia hali yake ya kawaida baada ya kumalizika kwa ukarabati kwa  sehemu maalum ya kuegesha feri katika kivuko hicho.

Akiongea na Radio Kaya afisa wa uhusiano mwema katika shirika la huduma za feri Haroon Mutiso amesema kuwa kuregelewa kwa huduma katika kivuko hicho kutasaidia kupunguza msongamano wa watu na magari uliokuwa unashuhudiwa mara kwa mara katika kivuko cha feri cha Likoni.

Mutiso aidha amesema kuwa hatua hiyo itaboresha huduma za usafiri hasa kwa watalii wanaoelekea Pwani kusini kupitia kivuko cha Likoni.

Afisa huyo wa uhusiano mwema katika shirika la huduma za feri amewataka wakaazi kuzingatia sheria za shirika la huduma za feri wanapotumia kivuko hicho ili kuepuka changamoto za uchukuzi.

Taarifa na Hussein Mdune. 

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.