FKF kutafutia ufadhili ligi ya soka Pwani

April 23, 2018

Shirikisho la soka nchini FKF tawi la Pwani kusini limeidhinisha mikakati ya kutafuta wawekezaji wa kibinafsi na viongozi wa kisiasa kutoa udhamini kwa timu zinazoshiriki ligi kuu ya Pwani Kusini (FKFSCB).

Mwenye kiti wa tawi hilo Gabriel Mugendi amesema kwamba timu nyingi za zinapitia changamoto kubwa ya ukosefu wa fedha za kujisimamia kwenye ligi hiyo.

Akizungumza baadaya kukutana na wadau wa soka wa Pwani Kusini Mugendi amesema kwamba tayari ameanzisha mikakati ya kutafuta wawekezaji wa kibinafsi watakaotoa ufadhili kwenye ligi hiyo.

“Nahitaji karibia milioni 7 kuweza kuendesha ligi hii. Na ni lazima nione kwamba nimezipata hizi milioni 7 ili kusiwe na changamoto yoyote,” amesema Mugendi.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.