Gavana aanzisha vita dhidi ya ndoa za mapema

June 8, 2018

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi amepinga vikali ndoa za mapema.


Akizungumza katika hafla ya kuwatuza wanafunzi waliofanya vyema katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini, Kingi amesema kuwa pamoja na kamishna wa kaunti ya Kilifi wamepiga marufuku disco matanga ili kumwokoa mtoto wa kilifi.

Kingi amesema kuwa wameafikia hatua hiyo baada ya kutambua kuwa  idadi ya visa vya mimba za mapema vipo  juu katika kaunti ya Kilifi.

Aidha amewatahadharisha wazazi dhidi ya kuwaachilia watoto wao ili kushiriki katika shughuli za maombolezi.
Gavana Kingi amezidi kusema kuwa serikali ya kaunti yake itazidi kuimarisha shule za chekechea ili kuboresha viwango vya elimu katika kaunti hiyo.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.