George Okong’o ateuliwa rasmi kama mkurugenzi wa KMA

October 12, 2018

Bodi ya Halmashauri ya Baharini nchini KMA imemteu rasmi George Okong’o kama mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo.

Kulingana Mwenyekiti wa bodi hiyo Malika Ali, mkurugenzi huyo mpya atahudumu kwa kandarasi ya miaka 3.

Okong’o amechukua nafasi ya aliyekuwa Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka hiyo George Magoya ambaye kipindi chake cha kuhudumu kilikuwa kimekamilika..

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu huyo mpya George Okong’o amefurahishwa na uteuzi huo, akisema atashirikiana vyema na mamlaka hiyo ili kuhakikisha inaimarika zaidi.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.