Haki Afrika yalaani vikali mauaji ya bodaboda Likoni

November 1, 2018

Shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la Haki Afrika limekashifu vikali mauaji ya Mohammed Abdulrahman mhudumu wa bodaboda katika eneo la Likoni.

Mkurugenzi wa shirika hilo Hussein Khalid amesema kwamba Abdulrahim mwenye umri wa miaka 34 aliuawa mapema siku ya Jumatano akiendeleza shughuli zake za kikazi.

Khalid ameitaka mamlaka ya kutathimini utendakazi wa maafisa wa polisi IPOA kuidhinisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo baada ya kudaiwa kwamba mhudumu huyo aliuawa na maafisa wa polisi.

Mtetezi huyo wa haki amewataka maafisa wa polisi kukomesha tabia ya kuwaua washukiwa badala yake wafuate utaratibu ulioorodheshwa kisheria.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.