Hakuna anishindaye isipokuwa Michael Jackson – Diamond Platinumz

December 4, 2018

Msanii wa Bongo flava Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz amefunguka na kusema kuwa hakuna msanii anayemshinda isipokuwa marehemu Michael Jackson.


Msanii huyo amesisitiza kuwa kila anapopanda juu ya jukwaa kuwatumbuiza mashabiki wake yeye hulenga kuwapa burudani ambalo hawajawahi kuliona kwengine na ndio maana yeye ni bora kuliko msanii yoyote yule.

Diamond Platinumz ni mmoja wa wasanii wanaofanya vyema zaidi Afrika Mashariki.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.