Hamasa dhidi ya seli mundu yazinduliwa Mombasa

June 19, 2018

Serikali ya Kaunti ya Mombasa imezindua hamasa kuhusiana na ugonjwa wa ‘Seli-Mundu’ yaani Sickle Cell ili kuwawezesha wagonjwa kupata tiba maalum, ushauri na usaidizi wa kiafya ili kuondoa maumivu na mahangaiko.

Mkurugenzi wa huduma za afya katika Kaunti ya Mombasa, Daktari Shem Patta, ameutaja ugonjwa huo kama unaowaathiri watu wazima na watoto japo wakaazi wengi hawaufahamu wala kujua athari zake kiafya.

Akiwaongoza wakaazi katika maadhimisho ya siku ya maradhi ya ‘Seli-mundu’ ulimwenguni yaliyofanyika katika eneo la Portreitz huko Changamwe, Daktari Patta amesema kwamba maradhi hayo hula chembechembe za damu na hata kupelekea kuziba kabisa kwa mishipa ya damu hivyo basi kumuweka mgonjwa katika hatari.

Daktari Patta amesema kwamba ugonjwa huo umebainika kuchangia vifo vingi vya watoto waliyo hini wa umri wa miaka mitano katika mataifa ya Afrika Kenya ikiwa moja wapo ya mataifa hayo.

Amesisitiza umuhimu wa wagonjwa kutafuta ushauri wa kimatibabu na kuzingatia maagizo ya Watalam wa afya ili kudhibiti ugonjwa huo ambao kamwe hauna sababu maalum kuhsuu maambukizi yake.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.