Harambee starlets kukosa AWCON

November 8, 2018

Kikosi cha Harambee Starlets sasa huenda kikakosa kushiriki mchuano wa AWCON baada ya Equatorial Guinea kushinda rufaa ya kesi yakuondolewa kwao kutoshiriki mashindano ya kinadada nchini Ghana.

Kenya ilikuwa imeshinda kesi dhidi ya Equatorial Guinea mbele ya kamati ya nidhamu lakini sasa bodi ya rufaa ya CAF imebadilisha uamuzi huo. Uamuzi wa bodi hiyo kunaifanya Equatorial Guinea kurudi mashindanoni.

Hii  inamanisha Kenya haitoshiriki kipute hicho nchini Ghana.

Kenya ilikuwa imewasilisha kesi dhidi ya Equitorial Guinea baada ya utumizi wa mamluki kufanywa na Guinea.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.